Home Uncategorized SIMBA KUMBE YAWATISHA WAZIMBABWE KIMTINDO

SIMBA KUMBE YAWATISHA WAZIMBABWE KIMTINDO

 


ILE kauli mbiu ya Simba kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ijulikanayo kama War in Dar, kwa kiasi fulani imeonekana kuwatisha Wazimbabwe hao.

 

Hiyo ni baada ya Kocha Mkuu wa FC Platinum, Norman Mapeza, kuibuka na kusema kwamba mchezo wao marudiano hautokuwa rahisi kutokana kufuatilia rekodi ya Simba katika mechi zake za nyumbani kwenye Ligi Mabingwa Afrika ambazo zinawatisha.


Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumatano iliyopita ijini Harare, Zimbabwe, FC Platinum iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Januari 6, mwakani ambapo mshindi wa jumla anafuzu hatua ya makundi, huku atakayepoteza akiangukia hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mepeza alisema: “Ukweli uliowazi ni kwamba, wamekuwa na rekodi nzuri katika uwanja wao wa nyumbani, hilo jambo kiasi fulani linatia hofu lakini bado haiwezi kutukwamisha kusimamia mipango yetu, tumeshinda nyumbani lakini hata nje ya hapa bado tunahitaji matokeo bora.


“Kuhusu kuwafuatulia wapinzani, kwetu linafanyika bila shida na ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuanza maandalizi mapema, ” .

 

Simba imekuja na kauli mbiu hiyo ikiwa na maana kwamba vita ipo jijini Dar katika mchezo huo wa marudiano ambapo wachezaji wameahidi kucheza kwa uwezo wao wote ili kufuzu hatua ya makundi.

SOMA NA HII  SIMBA YAANZA KUIWINDA LIPULI, MZUNGU AZITAKA POINTI TATU