Home Uncategorized WAPINZANI WA SIMBA WAWASILI, WAPOKELEWA KWA NYIMBO

WAPINZANI WA SIMBA WAWASILI, WAPOKELEWA KWA NYIMBO


 TIMU ya Plateau United imewasili leo Desemba 4 ikitokea nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kesho wa marudio dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.


Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni wa hatua ya awali unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote mbili zinasaka nafasi ya kusonga hatua ya mtoano ili kuweza kufikia hatua ya makundi.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Nigeria, Novemba 29, Simba ilishinda kwa bao 1-0 ikiwa ugenini ina kibarua cha kulinda ushindi wake ikiwa nyumbani.

Plateau United ilipokelewa na mashabiki wake wa Tanzania ambao walikuwa wamevaa jezi za njano ambao waliwapokea kwa kuwaimbia nyimbo.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR LEO DHIDI YA SIMBA UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO