Home Uncategorized MBEBA MIKOBA YA JONAS MKUDE, MAJANGA MATUPU

MBEBA MIKOBA YA JONAS MKUDE, MAJANGA MATUPU


 MZAMIRU Yassin kiungo mkabaji wa Yanga anatajwa kupewa mikoba ya Jonas Mkude leo Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Platinum. 


Mkude amesimamishwa na Simba kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu huku ingizo jipya Taddeo Lwanga ambaye ni mbadala wake akisumbuliwa na majeraha.

Lwanga ambaye ni kiungo mkabaji raia wa Uganda amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Simba ila inaelezwa alipata majeraha wakati Simba ikijiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Majimaji.

Kwa sasa mikoba ya Mkude inaelezwa kuwa atapewa kiungo mzawa Mzamiru ambaye atafanya kazi kwa ushirikiano na nyota Said Ndemla.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote ndani ya kikosi hicho wana uwezo mkubwa wa kumpa matokeo.

“Kila mchezaji ndani ya timu ana uwezo mkubwa na anafanya kazi kwa ushirikiano, ni jambo la kusubiri na kuona kwamba tunapata matokeo ndani ya uwanja,” .

SOMA NA HII  LIGT AUNGANA NA CR7 JUVENTUS, ASAINI MIAKA MITANO