Home Uncategorized SIMBA: KAMA MWARABU ALIKUFA KWA MKAPA FC PLATINUM HAWATOKI

SIMBA: KAMA MWARABU ALIKUFA KWA MKAPA FC PLATINUM HAWATOKI


 UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa hakuna sababu ya kushindwa kuwafunga Platinum FC kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utachezwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa.

 Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wana historia kubwa kwenye mashindano hayo na kwamba timu kubwa kama As Vita, Al Ahly, JS Soura na timu zingine zilifungwa kwa Mkapa itakuwaje washindwe kuwafunga Platinum.

 

Manara amesema maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo yapo tayari kwa asilimia 100 na timu hiyo ilipasha misuli moto kwenye Uwanja wa Mkapa na jana walikuwa kwenye uwanja wao wa Mo Simba Arena kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.


“Ombi letu tulilopeleka Shirikisho la Soka Afrika (Caf ), la mchezo kurudishwa nyuma kutoka saa 1:00 usiku hadi saa 11:00, limekubaliwa.

 

“Kwa hiyo mchezo upo palepale na utapigwa saa 11:00 za jioni pale kwa Mkapa. Tuliomba muda irudishwe nyuma kutokana na miundombinu ya mji wetu tunataka watu waje na wawahi kurudi makwao.

 

“Nitumie nafasi hii kuwaambia Wanasimba wote na Watanzania, Simba tunakwenda kuweka rekodi ya kufuzu kucheza hatua ya makundi kwa mara ya pili kwenye nchi hii, hakuna timu nyingine yoyote ya Tanzania tangu dunia hii iumbwe sisi ndiyo tunakwenda kuwa wa kwanza.

 

“Kama Nkana, As Vita, Al Ahly, Js Soura na hao wengine walikufa hapa Dar es Salaam, hao Platinum ni akina nani. Hawatoki kivyovyote vile, lazima waondoke, lakini hii itachagizwa vikubwa na uwepo wa mashabiki na sapoti ya Watanzania wote.


“Punguzo la tiketi kutoka shilingi 7,000 hadi 5,000 kwa mzunguko kama ambavyo tulitangaza, inatarajiwa kumalizika 5:59 usiku wa leo (jana), wakati zile za V.I.P A na B ambavyo ni shilingi 40,000 na 100,000, zitabaki kama zilivyo.

 

 “Ile War In Dar ilikuwa na maana ya kuhamasisha kupigana kufa na kupona ndani ya uwanja dakika 90 kusaka ushindi. Siyo vurugu wala vita ya mabunduki, vita ni pale wanaume 22 watakapokwatuana uwanjani.

SOMA NA HII  MBADALA WA MROMANIA WA AZAM FC AANZA KAZI CHAMAZI

 

“Kwetu sisi huu mchezo una umuhimu zaidi ya watu wengine wanavyofikiria, tunataka historia na rekodi mpya kwenye nchi hii, narudia kusema tunataka kwenda hatua ya makundi kwa mara nyingine tena. Mashabiki wakiimba War In Dar kwa dakika zote 90, wale Platinum wanatokaje, alikufa Mwarabu hapa,” alisema.