Home Uncategorized WEST HAM UNITED YAINGIA ANGA ZA ARSENAL

WEST HAM UNITED YAINGIA ANGA ZA ARSENAL

 


NYOTA wa Klabu ya Arsenal, Eddie Nketiah anatajwa kuingia Kwenye rada za Klabu ya West Ham United ambayo inahitaji kumpata mbadala wa Sebastien Haller kwa mujibu wa ripoti.


Haller ameweka rekodi ya ada ya usajili ndani ya West Ham United ambao ni pauni milioni 22 na ameibukia ndani ya Klabu ya Ajax baada ya usajili wake kukamilika Ijumaa.


Hesabu za West Ham United kuipata saini ya Nketiah mwenye miaka 21 ni pendekezo la Kocha Mkuu, David Moyes ambaye anataka kuboresha kikosi chake.


Pia kutopata namba kikosi cha kwanza ndani ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kunampa imani ya kumpata mchezaji huyo kwa kuwa ameanza kwenye michezo mitatu pekee ndani ya Ligi Kuu England msimu huu kutokana.

 Nafasi yake ndani ya uwanja ambayo ni ushambuliaji imekuwa na ushindani kwa nyota Alexandre Lacazette na nahodha Pierre Emerick Aubameyang ambao ni chaguo la kwanza la kocha.

SOMA NA HII  MWAMBA WA LUSAKA AMEPATWA NA NINI SIMBA