HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja amesema kuwa kwa kuwa wameanza na taji la Mapinduzi 2021, makombe mengine yanakuja zaidi.
Nyota huyo alikuwa ni nahodha visiwani Zanzibar na alikiongoza kikosi kwenye mechi zote nne ndani ya uwanja, ambapo kwenye dakika 360 walifungwa bao moja na kufunga mabao mawili.
Mabao hayo mawili waliifunga Namungo bao moja na sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC huku yeye akitengeneza pasi zote za mabao.
“Kazi kubwa ilikuwa ni kupambana kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, huu ni mwanzo ni muda wa kuendelea kuwa na furaha, mashabiki waendelee kutupa sapoti, makombe mengine yanakuja”.