Yanga SC

YANGA:MAKOMBE MENGINE YANAKUJA

admin January 18, 2021 5:47 am

 HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja amesema kuwa kwa kuwa wameanza na taji la Mapinduzi 2021, makombe mengine yanakuja zaidi.

Nyota huyo alikuwa ni nahodha visiwani Zanzibar na alikiongoza kikosi kwenye mechi zote nne ndani ya uwanja, ambapo kwenye dakika 360 walifungwa bao moja na kufunga mabao mawili.

Mabao hayo mawili waliifunga Namungo bao moja na sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC huku yeye akitengeneza pasi zote za mabao.


“Kazi kubwa ilikuwa ni kupambana kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi,  huu ni mwanzo ni muda wa kuendelea kuwa na furaha, mashabiki waendelee kutupa sapoti, makombe mengine yanakuja”.
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU KIKOSI CHA KWANZA CHA YANGA BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI WA FISTON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply