ZAKARI Thabit, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kurejea kambini kuendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
Mabingwa hao mara tano wa Kombe la Mapinduzi waliweka kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar ambapo huko walicheza mechi tatu za kirafiki pia wametinga hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho.
Katika mechi hizo walishinda mbili na kupoteza mechi moja ilikuwa kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya KMKM na walishinda mbele ya Mlandege mabao 2-0 na Zanzibar Combine 2-1.
Thabitb amesema:-“Wachezaji wa Azam FC wamepewa mapumziko baada ya kumaliza program yao Zanzibar watarejea kambini Jumatatu.
“Bado mechi nyingine za kirafiki zinahitajika kutoka nje ya Bongo ambapo Lusaka Dynamo kutoka Zambia itakuja ni mwalimu amependekeza iwe hivyo kwa uimara wa kikosi.
“Pia kuna mazungumzo na timu moja ya Uganda ambapo mazungumzo yakikamilika nayo itakuja kucheza mchezo wa kirafiki, lengo ni kuwa imara ili Ligi Kuu Bara ikirudi nasi tuwe na kasi,” .