Home Simba SC LOKOSA IS RED..!!

LOKOSA IS RED..!!


Simba SC leo Januari 25 wamemtambulisha rasmi mshambuliaji wao toka Nigeria, Junior Lokosa ambaye aliwasili nchini Jumamosi Januari 23.

Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii ya Simba wamemtambulisha pamoja na kuweka picha zake akiwa ana saini mkataba.

Lokosa ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwenye kipengele cha wachezaji watakaotumika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba itakutana na AS Vita, Al Ahly na Al Merrikh.

Simba wameweka ujumbe unaosomeka “Chuma toka Nigeria na mchezaji wa zamani wa EspĂ©rance kipo tayari Msimbazi na dili lake yake limekamilika. Lengo kuu ni nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku lengo mama likiwa Ligi Kuu na Kombe FA,”

Wameongeza kuwa “Simba Super Cup inakusubiri kwa hamu kubwa,”

Lokosa ataanza kuonekana kwenye mechi ya Simba Super Cup kuanzia Januari  27-31 jijini Dar.

SOMA NA HII  'MAVITUZI' YA OUATTARA YAMTIA WAZIMU ZORAN...AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOMTUMIA KIMKAKATI KUMALIZA 'KAZI CHAFU'...