Home Yanga SC YANGA YAWATANGAZA RASMI NIZAR, NA KOCHA MGHANA

YANGA YAWATANGAZA RASMI NIZAR, NA KOCHA MGHANA


KATIKA harakati za kuimarisha zaidi benchi lao la ufundi kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Klabu ya Yanga leo imewatangaza rasmi makocha wao wawili wapya ambao Nizar Khalfan na  Edem Mortotsi.

Nizar anakuja kuchukua nafasi ya kocha msaidizi iliyoachwa wazi na kocha Juma Mwambusi huku Mortotsi yeye akija kuchukua majukumu ya ukocha wa viungo pamoja na utimamu wa mwili nafasi ambayo ilikuwa wazi tangu kuondoka kwa Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini.

Makocha hao wawili sasa wataanza kazi rasmi chini ya Kocha Mkuu Mrundi, Cedric Kaze katika kambi ya kikosi hicho iliyoko Avic Town Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza baada ya utambulisho huo Mkurugenzi wa uwekezaji wa Klabu ya Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Usajili, Injinia Hersi Said amesema: “Tuna imani kubwa na mchakato uliofanyika na kufanikisha kupatikana kwa makocha hawa wawili, kama unavyowaona wote ni vijana na wana wasifu mzuri ambao ni wazi utakuwa msaada mkubwa kwenye timu yetu katika kufikia malengo tuliyojiwekea.”

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI...NTIBAZONKIZA AIBUKA NA LAKE YANGA...AMTUPIA MPIRA NABI...