Simba SC

LOKOSA ATOA KAULI YA KIBABE SIMBA

admin January 27, 2021 11:47 am


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba raia wa Nigeria, Junior Lokosa amefunguka kuwa malengo yake makubwa ya kujiunga na Simba ni kuja kushinda mataji kwenye michuano yote iwe ya ndani au ile ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa na kutambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Simba siku ya Jumatatu ambapo amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Esperance ya Tunisia aliyoitumikia msimu uliopita.

Akizungumzia malengo yake bada ya kusajiliwa na Simba Lokosa alisema: “Nina furaha kwa kuweza kukamilisha usajili wangu ndani ya kikosi cha Simba, hii ni heshima kubwa kwangu.

“Kuhusiana na matarajio nisingependa kusema mengi lakini naahidi kujituma kwa uwezo wangu wote kuhakikisha naisaidia Simba kuwa mabingwa wa Afrika kwa kushinda taji la Ligi ya mabingwa Afrika, lakini pia kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania.

“Najua mashabiki wa Simba wanatarajia mambo mengi kutoka kwangu, naamini taratibu nitaweza kuwafurahisha kwa kuionyesha kiwango cha juu,”

KILA LA KHERI TAIFA STARS LEO PAMBANENI KUFANYA KWELI YANGA YAWATANGAZA RASMI NIZAR, NA KOCHA MGHANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply