Home Uncategorized HAWA HAPA NYOTA TISA WA YANGA KUIKOSA SIMBA KOMBE LA MAPINDUZI

HAWA HAPA NYOTA TISA WA YANGA KUIKOSA SIMBA KOMBE LA MAPINDUZI


 HAWA hapa wachezaji wa kikosi cha Yanga wanaotarajiwa kukosekana kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi ambao ni fainali dhidi ya Simba.

Yanga ilitinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo ambao dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Hawa hapa wanatarajiwa kuikosa dabi ya leo:-

Bakari Mwamnyeto ana matatizo ya kifamilia.


Carlos Carlinhos anasumbuliwa na majeraha.

Mapinduzi Balama yupo Afrika Kusini akiendelea na matibabu..

Lamine Moro alipewa mapumziko kwa muda wa wiki mbili.

Yassin Mustapha, Deus Kaseke,Ditram Nchimbi, Feisal Salum na Farid Mussa hawa walikuwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ilibanana jana na timu ya Taifa ya Congo kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  JOSE MOURINHO ATOA SAPOTI KWA WAZEE WALIOPO KARANTINI