Home Simba SC KOCHA MAZEMBE : NITAMCHUKUA LARRY BWALYA KUTOKA SIMBA..!!

KOCHA MAZEMBE : NITAMCHUKUA LARRY BWALYA KUTOKA SIMBA..!!

KOCHA Mkuu wa Timu ya TP Mazembe, Felix Mwamba amesema kikosi cha Simba kimejaa wachezaji wengi wazuri lakini akiambiwa kuchagua mmoja kati yao atamchagua Larry Bwalya.

Mwamba ameyasema hayo leo wakati wakijinadi kuelekea mchezo wa kesho wa Simba Super Cup dhidi ya Simba.

Amesema Bwalya Ni mchezaji wa kumtizama kwa jicho la ziada unapocheza nae kwa kuwa ana vitu fulani ambavyo vinahitaji umakini zaidi ili kuvigundua.

“Wachezaji wa Simba ni wazuri sana kila mmoja kwa nafasi yake lakini Bwalya ni zaidi sana anajua nini anakifanya awapo uwanjani, “amesema Mwamba.

Amesema katika mchezo wao wa kesho wa kuhitimisha michuano hiyo mifupi watahakikisha wanapambana kupata matokeo.

Amesema Simba sio timu ndogo hivyo hata yeye kikosi chake anakiamini hana shaka na mchezo huo licha ya matokeo kuwepo ya aina tofauti na kocha anavyopanga.

Aidha Mwamba amesema, Simba Super Cup itamsaidia katika michuano ya Klabu bingwa ambayo timu yake inashiriki.

“Japokuwa imekuwa ya muda mfupi lakini imekuwa na umuhimu mkubwa sana kwetu sisi na hata hao Simba ambao wameandaa, “

Simba Super Cup inafikia tamati kesho katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo Mwekezaji wa Klabu hiyo Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema watahakikisha mashindano hayo yanakuwa endelevu kwa manufaa ya Simba na wanasimba wote kwa ujumla.

Amesema awamu ijayo watajitahidi kuongeza idadi ya timu huku akiwataka wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani kukiwa na jambo kama hili kipindi kingine.

SOMA NA HII  HUU NDIO UBAYA WA JEZI NO 20 YA CHA MALONE...MASTAA SIMBA WAKAE CHONJO.....