Home Uncategorized MASHABIKI WATANO WASEPA NA MKWANJA KUTOKA M-Bet

MASHABIKI WATANO WASEPA NA MKWANJA KUTOKA M-Bet


  JUMLA ya wa wanamichezo watano wameshinda kiasi cha Sh 86,844, 530 baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 za ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya Perfect 12 ya kampuni ya M-Bet.

Washindi hao  wamepatisakana katika droo ya M-Bet iliyofanyika Januari 6 jijini kwa mujibu wa Ofisa Habari wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley.

Malley aliwataja washindi hao kuwa ni Charles Hamis, Isihaka Mombo (Njombe), Titus Mguli (Njombe), Eric Mosha (Tanga) na Baltazary Saunary wa Arusha.

Malley amesema kuwa kupatikana kwa washindi hao kunafanya droo ya 101 kutokea kuanzishwa kwa Pefect 12 ambayo ni nyumba ya mabingwa.

Amesema kuwa M-Bet inajivunia kuendelea kubadili maisha ya Watanzania kupitia michezo yake mbalimbali na kuwaomba watanzania wenye vigezo vya kufanya hivyo kuanza kujaribu bahati yao.

“Sisi tunaendelea kuwa nyuma ya mabingwa na kuwainua vipato Watanzania, mpaka sasa kuna washindi wengi wamefaidika na michezo yetu na kuweza kubadili maisha yao,” amesema Malley.

Mmoja wa washindi hao, Charles Hamis kutoka Lindi amesema kuwa amefurahi sana kushinda kiasi cha fedha hicho kwa kutumia Sh 1,000 tu kubahatisha.

Hamisi ambaye shabiki wa timu ya Simba na Manchester United amesema kuwa awali alidhani kuwa michezo ya kubahatisha ni ‘dili’ lakini baada ya kuona mashabiki kibao wakishinda kupitia M-Bet, naye aliamua kubashiri.

“Sikukata tamaa kutokana na ukweli kuwana watu wangu wa karibu walikuwa wanashinda kiasi cha fedha kupitia mchezo wa Perfect 12, niliamini kuwa kuna siku nami nitashinda,” amesema Hamis.

Kwa upande wake,  Mguli ambaye ni shabiki wa Simba na Chelsea amesema kuwa atatumia fedha hizo kuendeleza biashara zake na kuinua kipato.

SOMA NA HII  OLE GUNNER: FERNANDES KAMA RONALDO