Home Simba SC MORRISON AWEKA REKODI TATU KWA MKAPA KAMA NAMBA YA JEZI

MORRISON AWEKA REKODI TATU KWA MKAPA KAMA NAMBA YA JEZI


NYOTA wa kikosi cha Simba, Bernard Morrison ameweza kuweka rekodi tatu za ajabu ndani ya Uwanja wa Mkapa kama namba yake ya jezi inavyosoma mgongoni.

Nyota huyo anaweka rekodi ya kwanza kuwa nyota wa kwanza kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu na kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano pamoja na ile staili ya kushangilia huku mpira ukiwa ndani ya bukta.

Morrison ameweka rekodi yake ya kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu ilikuwa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Simba Super Cup, Januari 27 ambapo alifunga bao la kwanza dakika ya 86 ambapo alishangilia kwa kuweka mpira ndani ya bukta na lile la pili alifunga dakika ya 89.

Pia ndani ya dakika 27 ambazo alitumia Morrison akitokea benchi kwa kuchukua nafasi ya Francis Kahata aliweza kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 90+3.

Morrison amesema:”Ninafurahi kufunga na ninapenda kuwa na furaha ndani ya Simba, nina amini mashabiki wanapenda kuona tunafanya vizuri hivyo tutazidi kupambana,”.

Leo Simba ina kazi ya kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa pili ambao ni wa kilele cha Simba Super Cup dhidi ya TP Mazembe.

SOMA NA HII  FARID MUSSA 'ASUKUMIWA' SIMBA....MABOSI YANGA WAMPA UKWELI KUWA HATAKIWI....