Home Uncategorized NAMUNGO WAREJEA BONGO

NAMUNGO WAREJEA BONGO

 


KIKOSI cha Namungo FC kimewasili leo Januari 6,2020 salama kwenye ardhi Dar es Salaam kikitoka Sudan.


Jana Januari 5 kilikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho wa marudio dhidi ya Al Hilal Obeid ambapo ililazimisha sare ya kufungana mabao 3-3.


Sare hiyo inaifanya timu hiyo iwaondoshe wapinzani hao kwa jumla ya mabao 5-3.


Mchezo wa kwanza waliocheza Uwanja wa Azam Complex,  Namungo FC ilishinda mabao 2-0.

SOMA NA HII  VITA YA UFUNGAJI BORA ENGLAND IMEANZA KUPAMBA MOTO