Home Simba SC SAKATA LA JONAS MKUDE SIMBA HUKUMU IPO PALEPALE

SAKATA LA JONAS MKUDE SIMBA HUKUMU IPO PALEPALE

IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya Simba Jonas Mkude hukumu yake ipo palepale na kwa sasa anasubiri kupewa adhabu yake kutokana na makosa yake ya utovu wa nidhamu.

Kiungo huyo chaguo namba moja la makocha wote ambao wanapita ndani ya Simba kwa sasa yupo nje kidogo ya timu hiyo baada ya kusimamishwa mwishoni mwa mwaka 2020 kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

Habari zimeeleza kuwa licha ya Simba kugoma kuweka wazi makosa yake miongoni mwa sababu ambazo zilipelekea aweze kuwekwa kando ni pamoja na kuchelewa safari zote mbili za timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilikuwa ile ya kwenda Nigeria kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United.

Pia kwenye safari ya kwenda Zimbabwe ambapo ilipoteza Simba kwa kufungwa bao 1-0 na FC Platinum huku mtupiaji akiwa ni Perfect Chikwende ambaye kwa sasa ni mali ya Simba.

Mbali na hapo inaelezwa kuwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati wanakwenda Mbeya kumalizana na Mbeya City, Mkude alichelewa jambo lililofanya viongozi wa Simba kongea naye ili aweze kubadili mwendo wake ila mambo yakawa ni yaleyale.

Chanzo kimeeleza kuwa kwa wakati huu adhabu yake ya kwanza ilikuwa ni kukosa mechi 10 baada ya wachezaji wa Simba kuomba iwe hivyo na tayari ameshakosa mechi saba za mashindano.

Mechi moja ilikuwa ni Kombe la Shirikisho moja ya ligi na mechi nne zilikuwa ni za Kombe la Mapinduzi huku moja ikiwa ni ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mkude kwa sasa bado kesi yake inaendelea na hivi karibuni huku yake itatoka hivyo ni suala la kusubiri,” .

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema:”Suala la Mkude lipo kwenye kamati ya nidhamu muda ukifika wao watatoa majibu,”.

SOMA NA HII  SIMBA YAFANYA USAJILI MPYA LEO UPANDE MWINGINE KABISA