Home Uncategorized SIMBA YATAMBULISHA UTATU MATATA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA YATAMBULISHA UTATU MATATA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


UONGOZI wa Simba umetambulisha utatu mpya ambao utapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Imekuwa ikielezwa kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kaimu Kocha, Seleman Matola ipo kwenye mpango wa kumsajili nyota wa Klabu ya FC Platinum, Perfect Chikwende.

Winga huyo amekuwa maarufu ghafla baada ya kuitungua Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe. 

Nyota huyo amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ambayo imemalizana na mshambuliaji Mpianza Monzinizi kutoka FC Lupopo na kipa Mathias Kingonya.

Usajili wa kipa huyo unatajwa kuweza kumuondoa kipa mmoja ambaye ni David Kissu pamoja na mshambuliaji mmoja ambaye ni Richard Djod.

Ikiwa Chikwende atamalizana na Simba ataungana na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone na mshikaji wake Clatous Chama ambao wamekuwa wakifanya vizuri ndani ya Simba.

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Haji Manara, ameandika kuwa Chama +Chikwende + Miquissone =CCM


SOMA NA HII  SVEN ATAJA KINACHOISUMBUA TIMU YAKE KWA SASA