SIMBA YAPELEKWA MAHAKAMANI NA RWEYEMAMU
ALIYEWAHI kuwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, anaripotiwa kuishitaki timu hiyo mahakamani.
Inadaiwa kuwa, Rweyemanu ambaye aliondolewa Simba mwaka jana baada ya Simba kupata matokeo mabaya mfululizo sasa inaripotiwa anataka kusafishwa na kulipwa fedha ambazo anaidai timu hiyo ili wamalizane vizuri.
Mechi mbili mfululizo Simba iliyeyusha pointi sita ilikuwa kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Mwanasheria wake, John Feka, alikiri kuwepo kwa madai hayo ambayo yapo kwenye mahakama ya usuluhishi.
Feka amesema mteja wake ameitaka Simba kukanusha tuhuma zilizotolewa na timu ambazo zililenga kumchafua kwa makusudi.
โKweli kesi ipo mahakama ya usuluhishi na kikubwa ipo kesi ya madai ya fedha ambazo ni siri.
โKesi nyingine ya tuhuma ambazo amepewa mteja wangu zilitaka kumchamfua kutokana na tuhuma alizopewa,โ alisema wakili huyo.
Chanzo:Championi

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.