Ligi Kuu

KMC YATIA TIMU RUKWA, KAMILI KUIVAA TANZANIA PRISONS

admin February 10, 2021 6:47 am

TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, Jana, Februari 9 alfajiri ilisepa  jijini Dar es Salaam kuelekea Mkoani Rukwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa siku ya Ijumaa saa 8.00 mchana katika Uwanja wa Nelson Mandela.

Kikosi hicho cha wana Kino Boys kimewasili salama kikiwa na wachezaji 20, viongozi watano pamoja na benchi la ufundi.

Ni mara ya kwanza kwa KMC FC  kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Nelson Mandela. 

 KMC ipo Rukwa ikiwa imetoka kucheza mechi yake ya kiporo dhidi ya Namungo na kuweza kuibuka na  ushindi wa mabao 3-0  ina alama 25 huku ikiwa kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imeshacheza michezo 18 hadi sasa.

 Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kupata pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

“Tupo tayari na kila mchezaji ana morali ya kufanya vizuri ndani ya uwanja, hakuna majeruhi hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” .


AZAM FC KUMENYANA NA COASTAL UNION, LYANGA AREJEA NYUMBANI DAVID MOYES:TULISTAHILI KUFIKA HATUA YA PENALTI FA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply