GEORGE Lwandamina, mrithi wa mikoba ya Aristica Cioaba ndani ya kikosi cha Azam FC ndani ya Azam FC kwenye mechi tano za mwamzo matokeo ambayo ameyapata ni tofauti na mtangulizi wake aliyepita.
Lwandamina amesaini dili la mwaka mmoja ndani ya kikosi cha Azam FC una kipengele cha kuongeza mkataba ikiwa atafanya vizuri.
Akiwa ameongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi tano ambazo ni dakika 450 ameambulia ushindi mechi moja pekee na kichapo kimoja huku akilazimisha sare tatu tofauti na Cioaba ambaye alianza kwa ushindi mechi zake tano za mwanzo.
Cioaba alishuhudia mabao 9 ya kufunga na alifungwa mabao mawili na alikusanya jumla ya pointi 15 kwenye mechi tano za mwanzo.Amempoteza mrithi wa mikoba yake Lwandamina ambaye ameongoza mechi tano za ligi.
Kwenye mechi hizo tano za ligi, Lwandamina amekusanya jumla ya mabao 8 ya kufunga na ameshuhudia wachezaji wake wakiokota mabao 8 kwenye nyavu zake.
Wakati akisaka pointi 15, Lwandamina amekusanya jumla ya pointi 6 na kupoteza jumla ya pointi 9 akiziyeyusha mazima.
Za Cioaba zilikuwa namna hii:-Azam FC 1-0 Polisi Tanzania, Azam FC 2-0 Coastal Union, Mbeya City 0-1 Azam FC, Prisons 0-1 Azam FC, Azam 4-2 Kagera Sugar.
Hizi ni za Lwandamina:-Azam 2-2 Namungo, Azam 2-2 Ruvu Shooting, Polisi 0-1 Azam FC, Simba 2-2 Azam FC,Coastal Union 2-1 Azam FC.