Home news NAMUNGO: WAANGOLA WALITUFANYIA UHALIFU

NAMUNGO: WAANGOLA WALITUFANYIA UHALIFU


UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Namungo umesisitiza kuwa kile kilichofanywa na wenyeji wao nchini Angola, Clube Desportivo 1º de Agosto, si fitina za soka bali ni uhalifu wa kupanga ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Namungo ilirejea nchini jana usiku baada ya mchezo wao wa mtoano hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya de Agosto uliopaswa kupigwa juzi Jumapili kufutwa.

Mchezo huo ulifutwa baada ya kuibuka mvutano mkubwa, baada ya nyota watatu wa kikosi hicho pamoja na kiongozi mmoja kudaiwa wana maambukizi ya Corona.

Kufuatia mvutano wa mamlaka mbalimbali za nchi zote mbili kwa kushirikiana na Shirikisho la soka Afrika (CAF), mchezo huo ulifutwa ili kupisha uchunguzi wa sakata hilo chini ya kamati maalum ya CAF.

Akizungumzia sakata hilo, Ofisa habari wa Namungo Namlia amesema: “Timu imelazimika kurejea nchini bila wachezaji wake watatu na kiongozi mmoja ambao kimsingi kutokana na sheria za mamlaka ya afya wao wataendelea kubaki mpaka pale watakapokuwa wamepona.

“Tunaendelea kusubiria maamuzi ya CAF lakini kiukweli kitu walichokifanya wenyeji wetu sio fitina za mpira kama ambavyo watu wengi wanalichukulia, bali ni uhalifu wa kupanga ambao umeshirikisha mamlaka mbalimbali za nchi hiyo,”

SOMA NA HII  BAADA YA KUJIHAKIKISHIA UFALME SIMBA...KIBU DENIS NAYE AANZA KUTOA TAMBO...MATOLA AMSIKIA NA KUTIKISA KICHWA...