KESHO Jumapili, Arsenal ya Mikel Arteta itawakaribisha Manchester City iliyo chini ya Pep Guardiola kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa Uwanja wa Emirates ikitajwa kuwa ni vita ya pasi na mbinu ndani ya uwanja.
Kwa sasa Ligi Kuu England imekuwa na ushindani mkubwa hivyo jambo lolote linaweza kutokea kwa miamba hii itakapokutana ndani ya uwanja.
City ipo nafasi ya kwanza na pointi 56, imeweka rekodi ya kushinda mechi 12 zilizopita ndani ya Premier League anakutana na Arsenal iliyo nafasi ya 10 ikiwa inapambana kurudi ndani ya top six.
Manchester City inaonekana kucheza mpira wa pasi nyingi sawa na Arsenal ambapo jumla City imepiga pasi 15,665 na Arsenal imepiga jumla ya pasi 12,434.
Rekodi zinaonyesha kuwa wababe hawa ndani ya Premier League wamekutana mara 47, Arsenal imeshinda jumla ya mechi 23 na City mara 14 huku zikikusanywa sare 10.