KUELEKEA mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Desportivo 1o de Agosto utakaopigwa leo katika dimba la Azam Complex Chamazi, nyota wa Namungo walioachwa nchini Angola wametuma salamu wakiiombea timu hiyo ushindi.
Nyota hao ambao ni Lucas Kikoti, Hamis Mgunya, Fredi Tangaru na Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa klabu, Omary Kaaya walilazimika kubaki nchini Angola kutokana na mamlaka za nchi hiyo kusema walikuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Akizungumzia hali za nyota hao, kocha mkuu wa Namungo, Hemmed Morocco amesema: “Kuelekea mchezo wetu wa leo dhidi ya wapinzani wetu 1de Agosto kutoka Angola, nyota wetu waliosalia nchini Angola, wametutumia salamu za kheri na kutuombea ushindi.
“Kuhusu hali zao wote wametuhakikishia kuwa wapo salama, na wanatamani kurejea hata leo lakini inabidi wasubiri mamlaka za nchi hiyo ziwape ruhusa,”