Home Simba SC BAADA YA KUWAFUNGA…AL AHLY WAJIPANGA KUMNG’OA LUIS MIQUISSONE SIMBA

BAADA YA KUWAFUNGA…AL AHLY WAJIPANGA KUMNG’OA LUIS MIQUISSONE SIMBA

 


WAARABU wamechukizwa na kipigo. Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone dhidi ya Al Ahly linaelezwa kwamba limewafanya mabosi wa klabu hiyo ya Misri kutaka kumng’oa Konde Boy.

Luis alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wao wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwafanya Simba waongoze kundi A ikiwa na pointi sita.

Hii inakuwa sio kwa mara ya kwanza mchezaji huyu kuhitajika na klabu mbalimbali, lakini mabosi wa Simba wamekuwa wagumu kumuachia.

Pia inaelezwa ugumu wa mkataba wake unachangia mchezaji huyo kutoondoka kwani wakati anasajilkwa akitokea Ud Songo alisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu Msimbazi.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU...SIMBA WAVUNA ZAIDI YA BILIONI 1 ZA ZAWADI TU...MCHANGANUO HUU HAPA...