Home Uncategorized KOCHA WA KINDOKI AMPA ONYO AISHI MANULA KISA TAIFA STARS ‘AWE MAKINI’

KOCHA WA KINDOKI AMPA ONYO AISHI MANULA KISA TAIFA STARS ‘AWE MAKINI’


Kipa wa zamani wa Yanga, Juma Pondamali, amemshauri kipa wa Taifa Stars, Aishi Manula kuongeza jitihada langoni.

Pondamali amezungumza hayo ikiwa ni siku mbili zimepita tangu kusafiri kwa Stars kuelekea Misri kwa ajili ya michuano ya AFCON.

Ameeleza kwa kusema “Manula anapaswa awe makini zaidi langoni.

“Siku za hivi karibuni amekuwa akifungwa mabao ambayo huwezi tarajia, vema akaongeja jitihada.

“Pia namtakia kheri pamoja na Stars nzima kwenye mashindano hayo ambayo hatujashiriki kwa muda mrefu.”

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YASEPA NA POINTI TATU ZA IHEFU