Home Ligi Kuu BARAZA ASEPA NA TUZO YA KOCHA BORA BONGO

BARAZA ASEPA NA TUZO YA KOCHA BORA BONGO


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United ameibuka na tuzo ya kocha bora kwa mwezi Januari ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya VPL.

Baraza ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Charles Mkwasa wa Ruvu Shooting na Abdalah Mohamed,’Bares’ wa JKT Tanzania.

Kwa kutwaa tuzo hiyo anaungana na kocha wa Yanga, Cedric Kaze ambaye ametwaa tuzo hiyo mara mbili kwa mwezi Oktoba na Desemba huku Aristica Cioaba aliyekuwa Azam FC akitwaa tuzo hiyo Septemba.

Mkwasa alitwaa tuzo hiyo Novemba na kuwa mzawa wa kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 kutwaa tuzo hiyo kwa upande wa makocha.

Pia nyota Deogratius Mafie, mshambuliaji wa Biashara United ametwaa tuzo ya mchezaji bora akiwashinda wachezaji wenzake ambao ni Mohamed Issa wa Ruvu Shooting na Wallace Kiango wa Mwadui FC.

Wengine ambao wameshawahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na Prince Dube wa Azam FC mwezi Septembe,Tonombe Mukoko wa Yanga Oktoba John Bocco wa Simba Novemba na Saido Ntibazonkiza wa Yanga Desemba.

SOMA NA HII  REKODI ZA MECHI 10 ZA YANGA V KAGERA SUGAR