Home Ligi Kuu LIGI IMEGAWANYIKA KWA SASA VIPANDE VITATU

LIGI IMEGAWANYIKA KWA SASA VIPANDE VITATU


MWENDO ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/21 unakwenda kwa kasi sana jambo ambalo linafanya kila timu kuzidi kuwa imara.

Ushindani ambao umeonekana kwenye mzunguko wa kwanza ulikuwa mzuri. Kila mpenda michezo ameona namna ilivyo na hali hiyo inapaswa kuendelea wakati wote.

Wachezaji wamekuwa wakipambana kusaka ushindi ndani ya uwanja. Hilo lipo wazi kutokana na kila timu kuwa na uhitaji wa pointi tatu.

Ikiwa tupo kwenye mzunguko wa pili tayari tunaona kwamba kuna mgawanyiko wa vipande vitatu ndani ya ligi yetu ya Tanzania.

Kipande cha kwanza ni zile timu ambazo zinawania kutwaa taji la Ligi Kuu Bara. Hapa kila timu inapambana kupata pointi ndani ya uwanja ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kutwaa ubingwa licha ya kwamba kwa sasa kuna timu ambazo zimeanza mbio za kujiondoa kwenye kusaka ubingwa.

Ukitazama kuna timu ambazo zimeachwa kwa jumla ya zaidi ya pointi 20 na kinara wa ligi huku zikiwa zinapambana kufikia malengo yao ya kubaki ndani ya ligi.

Uzuri ni kwamba kwa sasa kwenye mzunguko wa pili kila timu ina nafasi ya kufanya vizuri licha ya kwamba hakuna ambaye ameweza kujihakikishia nafasi ya kushuka ama kuchukua ubingwa.

Hivyo kwa makundi ambayo yapo jambo lolote linaweza kutokea mwisho wa msimu licha ya kwamba wahenga walisema kwamba utakavyoanza ndivyo utakavyomaliza.

Kundi la pili ni lile ambalo halina presha na kushuka ligi wala kuchukua ubingwa wao hesabu zao ni kubaki ndani ya ligi. Hili nalo lipo kwa msimu wa 2020/21.

Hapa kitakachoweza kuziweka salama timu hizi ni kuzidi kupambana ili kushinda mechi zao kwani ikiwa wataanza mzunguko wa pili kwa kupoteza na nafasi zao zitazidi kuwa ngumu. 

Uzuri ni kwamba kwa sasa asilimia kubwa michezo inayochezwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia kwa Azam Tv hili linaongeza ushindani pamoja na nguvu kwa wachezaji kuzidi kupambana.

Jambo la msingi ni kila timu kwa sasa kujipanga kwenye mechi zilizobaki ili kupata matokeo chanya ambayo yatawapa pointi tatu zitakazowafanya waweze kubaki kwenye kundi ambalo wanalihitaji.

Kuna dakika 90 ndani ya uwanja kwa ajili ya kusaka pointi tatu ambazo ni muhimu kwa kila timu.Maandalizi mazuri yanahitajika ili timu iweze kupata pointi tatu muhimu.

Sapoti ambayo timu inapata kutoka kwa mashabiki ni muhimu kulipwa ndani ya uwanja.Kila timu inahitaji kumaliza ligi kwa mafanikio hivyo muda wa mwisho kujipanga ni sasa.

Kwa mechi hizi za mwisho pia ni muhimu kwa waamuzi kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa kuzingatia sheria. Nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa na wachezaji watatimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  JUDIKA : HUYU KAGERE NI MTU NA NUSU

Ukija kwa kundi la tatu ni lile ambalo lipo kwenye hatari ya kushuka daraja na kuweza kutoka kwenye ligi na kuibukia kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

Hilo lipo wazi kwani ni lazima timu zishuke na zipo ambazo zitapanda ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 ikiwa zitashindwa kufanya vizuri kwa msimu huu.

Kundi hili la tatu huwa linakuwa kwenye hali ngumu dakika za lala salama kutokana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuwa na presha kubwa.

Rai yangu ni wakati huu kabla hatujafika kwenye nafasi hiyo inatakiwa kuongeza juhudi ili kuweza kufikia malengo ambayo kila timu inahitaji kuyafikia.

Matokeo mazuri ndani ya uwanja pia yanategemea maandalizi mazuri hivyo muda ambao umebaki kwa sasa kabla ya ligi kuendelea utumike vizuri kwa ajili ya maandalizi.

Maandalizi mazuri ni silaha ya timu kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote kwani hapo ndipo ambapo mwalimu hupata kikosi cha kazi pamoja na kujua namna gani awatumie wachezaji wake.

Ligi yetu imezidi kufuatiliwa na wengi.Wapo marafiki zangu kutoka Afrika Kusini wamekuwa wakiniambia kwamba wanaona namna ligi inavyochangamka na kuleta ushindani.

Hili inabidi liwashtue wachezaji wale ambao wanacheza kwa juhudi kiasi. Wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi ili waweze kujiweka sokoni kwa kuwa wanafuatiliwa na wengi nje na ndani ya Tanzania.

Kufanya vizuri kwa timu ambazo zipo kwenye kundi la zile ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja kutaifanya timu hiyo iondoke kwenye daraja hilo na kuibuka kwenye daraja la timu ambazo hazina presha ya kushuka.

Zile ambazo zimekata tamaa nina amini kwamba zina uwezo wa kupata matokeo chanya hasa ukizingatia kwamba mchezo wa mpira muda wote upo wazi na kila timu ina nafasi ya kushinda.

Ipo wazi yule ambaye atajiaandaa vizuri na kutumia nafasi ndani ya uwanja ni rahisi kwake kushinda na kujiondoa kwenye nafasi ambayo yupo kwa wakati huo ndani ya ligi.

Wachezaji mna kazi ya kupambana kwa ajili ya mzunguko wa pili ambao ushindani wake siku zote huwa ni mkubwa kwa kuwa ni muda wa mavuno kwa kila timu.

Yule ambaye atashindwa kwenda na kasi itakuwa na ngumu kwake kubaki ndani ya ligi. Imani yangu ni kwamba kila kundi litaongeza juhudi ili kuweza kupata matokeo chanya.