Home news WAWAKILISHI WETU KIMATAIFA MNA KAZI YA KUFANYA KIMATAIFA

WAWAKILISHI WETU KIMATAIFA MNA KAZI YA KUFANYA KIMATAIFA


 FURAHA ya mashabiki ni kuona timu inapata matokeo mazuri ndani ya uwanja. Jambo hilo lipo kwa kila mmoja ambaye anapenda mpira kwa kuwa ushindi ni furaha.

Kila timu nina amini kwamba imeweza kufanya maandalizi mazuri na bado inaendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya mechi zijazo za kimataifa.

Haitakuwa kazi nyepesi ndani ya uwanja kupata matokeo chanya. Muhimu kwa sasa ni kufanya maandalizi mazuri ambayo yatakuwa na faida kwa wawakilishi wetu kimataifa.

Klabu ya Namungo FC wao ipo kwenye hatua ya 32 bora Kombe la Shirikisho. Jambo la msingi ni kuona kwamba inaweza kupata matokeo ugenini ili kuweza kuongeza hali ya kujiamini.

Mechi ya kwanza ya Namungo watakuwa ugenini nchini Angola ambapo ili kuweza kuongeza hali ya upambanaji itapendeza ikiwa watapata matokeo kwenye mchezo wao ujao.

Pia wanapaswa watambue kwamba wanakutana na timu imara na bora hilo inabidi likae kwenye akili zao pale watakapokwenda kusaka ushindi mbele ya 1 de Agosto ya Angola.

Namungo watakuwa na kibarua Februari 14. Nina amini kwamba ina nafasi ya kupata matokeo chanya hata ikiwa ipo ugenini kwani mpira kwa sasa umebadilika.

Kila timu ina nafasi ya kushinda hata ikiwa itakuwa ugenini jambo la msingi ni maandalizi na mipango makini.

 Simba ipo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupenya kwenye hatua za mwanzo walizoanza nazo ina kazi ya kusaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Kila timu kwa namna yoyote kwa sasa inahitaji pongezi kwa kuwa haikuwa rahisi kufika hapo ilipo. Uzuri ni kwamba kila mmoja anapata kile ambacho anastahili ndani ya uwanja.

Mipango makini iliyotumika awali inapaswa kuendelea kutumika na kuboreshwa pia katika kusaka ushindi kwani jambo linalohitajika ndani ya uwanja ni ushindi.

Imani yangu ni kwamba tayari benchi la ufundi limeweza kuona makosa ya timu hizi zote mbili zilipo kwenye upande wa mashindano ya kimataifa.

Namungo wao kwenye mechi za ugenini kwa msimu huu wakiwa wamecheza moja wameruhusu mabao matatu na kufunga mabao matatu.

Inamaanisha kwamba wanaweza kushinda pia wakiwa ugenini na wanafungika pia wakiwa ugenini. Katika hilo ni muhimu kila timu kuwa na hesabu ndefu kimataifa ili kupata matokeo chanya.

Matokeo mazuri kwenye mechi za mwanzo yataongeza nguvu kufanya vizuri kwenye mechi zijazo ambazo ni za marudio katika mashindano ya kimataifa.

Hivyo rai yangu ni kwamba hawa wawakilishi wetu wapambane ndani ya uwanja kusaka ushindi ambao utakuwa ni zawadi kwa mashabiki na wadau wa masuala ya mpira.

Kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi inaonekana ni matatizo kwa timu zote mbili ndani ya dakika 90 ambazo watakuwa wanapambana.

Mchezo wa kwanza unagawa dakika 90 za awali kisha ule wa pili ambao ni wa marudio unamaliza zile dakika 90 za pili na kukamilisha jumla dakika 180.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...TANZANIA PRISOSN WAKUMBUSHA YA KAGERA NA MBEYA CITY....

Kufanya vizuri kwa timu hizi mbili kimataifa kutafungua njia ya mafanikio kwa wachezaji binafsi pamoja na timu kiujumla katika harakati za kuweza kufikia mipango.

Simba ambao leo Februari 12 watakuwa na kazi ugenini mbele ya AS Vita ina kibarua cha kufanya kupata ushindi mbele ya AS Vita.

Ikumbukwe kuwa Simba iliwahi kukutana na AS Vita hatua ya makundi na ilinyooshwa mabao 5-0 ikiwa Congo hivyo ina kazi ya kwenda kupambana ili kufikia malengo yao.

Ukiweka kando wawakilishi wetu kimataifa pia kwa sasa tupo mzunguko wa pili kwenye ligi.

Hesabu nzuri kwa sasa kila timu kuanza maandalizi yake ili kujiweka tayari kwa ajili ya mechi zijazo ambazo huwa na ushindani mkubwa.

 

Mzunguko wa pili siku zote huwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji kushinda kwenye kila mchezo. Kwa zile ambazo zitashindwa kupata matokeo uwanjani zitakuwa na ugumu wa kuweza kubaki msimu ujao.

 

Kuna timu nne ambazo zitashuka daraja na mbili zina kazi ya kucheza play off hivyo ikiwa zitashindwa kupata matokeo chanya itakuwa ngumu kwao kusalia msimu wa 2021/22.

 

Pia kuna Ligi Daraja la Kwanza ambayo nayo pia inatarajiwa kurejea nako nina amini kwamba ushindani utakuwa ni mkubwa na kila timu itakuwa inahitaji ushindi.

Kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza ni ndoto ya timu nyingi ambazo zinashiriki ligi hiyo huku zikikosa mpango kazi mwendelevu kupata matokeo ambayo wanayapata.

 

Pia ikiwa zitapata nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao itapendeza.Zitakuwa na kazi ya kuongeza umakini kwenye kulinda nafasi zao ili zilete ushindani wa kweli ndani ya uwanja.

Kila timu ikichanga karata zake vizuri basi nafasi ya kupata matokeo chanya ndani ya uwanja kutaongeza hali kujiamini kwa mabeki, safu ya ushambuliaji na kiungo

 

Hakuna timu ambayo inapenda kupoteza ndani ya uwanja ila inatokea kwa sababu matokeo lazima yapatikane kwenye kusaka ushindi uwanjani.

Kwa wawakilishi wetu kimataifa ni jukumu lenu kujipanga ili kufanya vizuri kwenye mechi zenu zijazo ndani ya uwanja ili kuweza kusonga mbele.

Wakati ujao ni muhimu kujipanga ili kufanya vizuri kwenye mechi za mwanzo ili kuongeza hali ya kujiamini. Kila mmoja ni muhimu kuwa na mipango makini pamoja na utayari wa kufanya makubwa.

 Siri pekee ya kuweza kupata matokeo ndani ya uwanja ni maandalizi mazuri pamoja na wachezaji kukubali kufuata mbinu za mwalimu ndani ya uwanja

Kushindwa kupata matokeo ni kuwaachia maumivu mashabiki.Ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa juhudi ndani ya uwanja ili kupata matokeo mazuri.

Mashabiki furaha yao ipo kwenye kupata ushindi hivyo wachezaji kazi yenu ni kupambana ndani ya uwanja ili kuweza kutimiza kile ambacho mashabiki wenu wanapenda.