LEO Februari 12 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kinatarajiwa kumenyana na AS Vita, ya Congo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.
Gomes ameweka wazi kuwa anatambua mbinu za Kocha Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge ila atapambana kupata matokeo chanya ili kupata pointi tatu muhimu.
Hiki hapa kikosi ambacho kinatarajiwa kuanza leo mbele ya AS Vita ugenini:-
Aishi Manula
Pascal Wawa
Joash Onyango
Shomari Kapombe
Mohamed Hussein
Thadeo Lwanga
Mzamiru Yassin
Rarry Bwalya
Luis Miquissone
Clatous Chama
Meddie Kagere