Home Ligi Kuu BIASHARA UNITED YAVUNJA UTEJA MBELE YA MWADUI FC

BIASHARA UNITED YAVUNJA UTEJA MBELE YA MWADUI FC

 


BIASHARA United ya Mara wanapenda kuitwa Wanajeshi wa mpakani wamevunja rekodi ya ubabe wa Mwadui FC wa kuwatungua kila wanapokutana Uwanja wa Mwadui Complex katika mechi za Ligi Kuu Bara. 


Ikiwa chini ya Francis Baraza imekuwa kwenye mwendo mzuri msimu huu ambapo ipo ndani ya tano bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Februari 13, Biashara United ilishinda mabao 2-1, Uwanja wa Mwadui Complex na kufuta rekodi zote za nyuma kwa kuwa haikuwa na bahati kushinda mbele ya Mwadui ikiwa ugenini.

Kwa muda wa misimu miwili, Biashara United ilikuwa inashindwa kufanya biashara na Mwadui FC kila inapotua Uwanja wa Mwadui Complex. 

Walianza msimu wa 2018/19 dakika 90 zilikamilika kwa Mwadui 2-1 Biashara United na kuacha pointi tatu muhimu.

Walipokutana msimu wa 2019/20, msimu wa pili wa  Biashara United baada ya kupanda Ligi Kuu Bara ilichezea kichapo cha bao 1-0 na kuacha pointi tatu.

Msimu wake wa tatu imefuta uteja kwa kushinda kwa mabao 2-1 ndani ya dakika 90, Uwanja wa Mwadui Complex.

Mara ya tatu kukutana Uwanja wa Mwadui Complex,  Biashara United wamevunja mwiko na kusepa na pointi tatu muhimu ugenini.

SOMA NA HII  PIRA KODI LEO KUCHEZWA MBELE YA POLISI TANZANIA