Home Ligi Kuu BREAKING: SIMBA V YANGA YAPANGIWA TAREHE UPYA KWA MKAPA

BREAKING: SIMBA V YANGA YAPANGIWA TAREHE UPYA KWA MKAPA


BREAKING: TAARIFA iliyotumwa na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) leo Mei 16 ambayo ni ratiba ya Ligi Kuu Bara imeonyesha tarehe mpya ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao uliyeyuka mazima Mei 8, Uwanja wa Mkapa kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda.


Muda wa awali wa mchezo huo ulipangwa majira ya saa 11:00 ila muda mfupi kabla ya mchezo ratiba ilibdilishwa na kupelekwa mpaka saa 1:00 usiku jambo ambalo Yanga waligomea.

Yanga iliweka wazi kwamba ni lazima Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kufuata kanuni kwa kuwa mpango huo ulikuwa ni kinyume na taratibu kuhusu kubadilisha muda.

Sasa watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana tena Uwanja wa Mkapa, Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

SOMA NA HII  GEITA GOLD MABINGWA WA JUMLA LIGI DARAJA LA KWANZA