Home kimataifa DAVID MOYES:TULISTAHILI KUFIKA HATUA YA PENALTI FA

DAVID MOYES:TULISTAHILI KUFIKA HATUA YA PENALTI FA


 David Moyes, Kocha Mkuu wa West Ham United amesema kuwa wakati wakichapwa bao 1-0 dhidi ya Manchester United mchezo wa Kombe la FA walistahili kufika Kwenye hatua ya kupigiana penalti.


Moyes amesisitiza kuwa majeruhi wa kikosi cha Kwanza ndani ya West Ham United yamewapa nguvu Manchester United kupata ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford. 


Bao la Scott McTominay katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za awali kukamilika bila mshindi kupatikana liliwaondoa jumlauumla West Ham United kwenye mbio za kuweza kutinga hatua ya robo fainali na lilipachikwa dakika ya 97.

SOMA NA HII  BENZEMA: RONALDO 'KANILIA BUYU' TOKA NISHINDE TUZO YA BALLON d'Or ...