Home news GAUCHO ATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO CHA MABAO 6-0

GAUCHO ATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO CHA MABAO 6-0


NAHODHA wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ baada ya kuanza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza katika Ligi Kuu nchini Morocco amesema kuwa ni matokeo mabaya ambayo watayafanyia kazi.

 Ilikuwa ni kwenye mchezo wake wa kwanza akivaa uzi wa Chabab Atlas Khenifira Feminin alishuhudia timu yake ikipokea zigo la mabao 6-0 na AS-Far wakiwa ugenini.


Gaucho ambaye alicheza dakika zote 90 amesema sababu ya kuchapwa sita kwenye huo ni kutokana na golikipa wao namba moja Chaimae Chawni kupigwa kadi nyekundu dakika za mapema, lakini pia wapinzani wao hao walipata penalti mbili za haraka haraka.

Nyota huyo ambaye ni Mtanzania alikuwa akicheza timu ya Simba Queens alipewa jukumu la kuongoza mashambulizi kwenye timu hiyo akisaidiana na Rania Kostani na Nouhaila Oubail, wakitumia mfumo wa 4-3-3 kama ambao alikuwa anacheza akiwa na Simba, lakini dakika 90 ziliisha wakiwa vichwa chini.

Gaucho amesema: “Mpira una matokeo matatu, kwahiyo sisi tulipata matokeo hayo baada ya dakika 90. Kikubwa ninachoshukuru niliaminiwa na nikacheza kwa mara ya kwanza na kuweza kujua ugumu wa ligi upoje huku.


“Pia kipa wetu namba moja alionyeshwa kadi nyekundu mapema jambo ambalo lilituvuruga na wapinzani wetu walipata penalti mbili za harakaharaka,”.
SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI....MANARA AMSHUKIA BEKI WA SIMBA INONGA...ADAI ANAPENDA SANA 'SIFA ZA KIJINGA'..