Home Ligi Kuu DUH! KICHAPO CHA RUVU SHOOTING WADAI NI UZALENDO

DUH! KICHAPO CHA RUVU SHOOTING WADAI NI UZALENDO


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting amesema kuwa hawakuwa na lengo la kupoteza mbele ya Namungo ila wamefanya uzalendo kuwapa nguvu wapinzani wao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Namungo ikiwa Uwanja wa Majaliwa, Februari 7 ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na kusepa na pointi tatu muhimu.

Pointi hizo zimewatoa kwenye nafasi ya 15 ambayo walikuwa awali na pointi zao 18 na kuwapandisha mpaka nafasi ya 12 ikiwa imecheza jumla ya mechi 16 na pointi zake 21.

Ruvu Shooting inabaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 28 baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza ikiwa imecheza jumla ya mechi 18.

Bwire amesema:”Hatukuwa na lengo la kushindwa mbele ya Namungo ila ilikuwa ni uzalendo unajua Namungo inawakilisha nchi kimataifa sasa tumeamua tuwape nguvu ili waweze kufanya vizuri kimataifa.

“Sisi mwendo wetu ni kuendelea kupapasa na kusaka ushindi kwenye kila mechi, kikosi chetu ni bora hiyo ipo wazi, hivyo wachezaji wetu ninawapongeza pamoja na Namungo pia,” .

SOMA NA HII  REKODI ZA MWADUI FC V MWADUI MUDA WOTE NDANI YA LIGI KUU BARA, LEO WANAKUTANA