Home Yanga SC YANGA HAWATAMBUI JAMBO LOLOTE KUHUSU SIMBA KIMATAIFA

YANGA HAWATAMBUI JAMBO LOLOTE KUHUSU SIMBA KIMATAIFA




 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautambui chochote kuhusu Klabu ya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwa na mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Simba itashuka Februari 23 kumenyana na Al Ahy ya Misri mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi na utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hatambui jambo lolote kuhusu Simba kuwa na mchezo mpaka pale atakapofuatilia na kujifunza.

“Kuhusu Simba kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwa na mchezo sijafuatilia na bado sijajua hivyo mpaka pale nitakapojua namna walivyojiandaa pamoja na timu ambayo watacheza nayo. 

“Kwa kweli sijafuatilia kujua kwamba ni timu gani inacheza, hivyo kwa kuwa nimekumbushwa kuhusu Simba nitafuatilia.

“Katika hilo nipo kimya kwa kuwa sijui jambo lolote ambalo linaendelea.Kuhusu wao ninasema kwamba mashabiki wetu wa Yanga watupe sapoti ili tuendelee kupambana tunakwenda Tanga, tunakwenda Kilimanjaro tunakwenda kwenye Kombe la Shirikisho tuungane tukapambane.

“Nimejitoa kwa ajili ya timu yangu ya Yanga hivyo kuhusu timu nyingine siwezi kuifuatilia kwa kweli,” amesema.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza na imekusanya pointi 49.


SOMA NA HII  YANGA YAWATOA 'CHAMBO' MAYELE NA FEI TOTO...WAISIKITIA SIMBA KWA KUUNGA UNGA...