Home Yanga SC YANGA YAAMBULIA KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA AFRICAN SPORTS, CHAMAZI

YANGA YAAMBULIA KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA AFRICAN SPORTS, CHAMAZI

 


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa kichapo cha bao 1-0 walichokipata mbele ya African Sports Februari 6 ni sehemu ya mchezo.


Ikiwa Uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports safu ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro iliokota wavuni bao dakika ya 73.


Kipa namba moja Metacha Mnata haikuwa na chaguo baada ya mshambuliaji wa African Sports,  Adam Uledi kutupia bao la ushindi.


Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 licha ya Yanga kupambana kusaka ushindi ikiwa na nyota wao mpya, Fiston Abdulazack ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya ENPPI.


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa vijana wake walitengeneza nafasi nyingi ila walishindwa kuzitumia jambo ambalo watalifanyia kazi.


“Ni mchezo wa kirafiki ipo wazi, matokeo ya kufungwa hayatabadilika ila tumejifunza jambo na wachezaji pia wameonyesha juhudi ni sehemu ya matokeo,”.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AANZA NA KUTATUA TATIZO LA UBUTU WA SARPONG