epl

THIAGO AAMBIWA KWAMBA ALIPASWA KUCHEZA MANCHESTER UNITED

admin March 2, 2021 1:47 pm


 LEGENDI wa Klabu ya Manchester United Paul Scholes anaamini kwamba nyota mpya wa Klabu ya Liverpool, Thiago angefanya vizuri ikiwa angekuwa ndani ya Old Trafford.

Thiago Alcantara sio aina ya wachezaji ambao anawataka Jurgen Klopp jambo ambalo linamfaya ashindwe kwenda na kasi ya kikosi hicho ambacho kinatetea taji la Ligi Kuu England.

Hiyo ni kwa mujibu wa Scholes ambaye amesema kuwa kwa namna alivyomtazama nyota huyo wengi wanamlaumu bila kujua kwamba anatumika tofauti na uwezo wake.

Legendi huyo ameweka wazi kwamba alianza kumtazama Thiago tangu anatua ndani ya kikosi cha Liverpool baada ya kujiunga hapo akitokea Klabu ya Bayern Munich.

“Ni kiungo mzuri naona kwamba wengi wanamlaumu kutokana na kushindwa kuonyesha uwezo wake ila hajafeli kwa sababu anashindwa ila bado sio aina ya wachezaji wa Klopp.

“Kwa namna ambavyo Liverpool wanacheza mbele wakiwa watatu inakuwa ngumu kwake kwenda mbele zaidi anakuwa chini na haonekani hivyo bado mtindo wa Liverpool unamkataa.

“Nadhani labda angekuwa ndani ya Manchester United angepata nafasi ya kuwa imara na bora zaidi ila kwa sasa ni jambo la kusubiri,”.

MSHAMBULIAJI WA YANGA ATOA AHADI YA MABAO LUIS NA MANULA NI HABARI NYINGINE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply