KOCHA msaidizi wa klabu ya AS Vita ya nchini Congo, Raoul Shungu amesema kuwa yupo tayari kuisikiliza ofa ya Yanga kama watahitaji aje kuifundisha timu hiyo.
Yanga tayri imemtambulisha kocha Juma Mwambusi kama kocha wa muda wa timu hiyo, huku mchakato wa kumsaka mbadala wa Kaze aliyefutwa kazi Jumapili iliyopita ukiendelea.
Shungu mwenye uraia wa Congo DR, aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa mwaka 1998/99 na kuondoka mwaka 2001 na nafasi yake ilichukuliwa na kocha Boniface Mkwasa.
Akizungumzia mpango huo Shungu amesema: “Nimesikia kuwa aliyekuwa kocha mkuu kwa sasa hayupo, sijawasiliana na kiongozi yeyote wa Yanga juu ya kuwa kocha wao lakini kama watakuwa wananihitaji basi nitasikiliza ofa yao ipoje kwangu.
“Nishawahi kuwa kocha wa Yanga, mpira wa Tanzania naufahamu vizuri na changamoto zake nafurahi niliishi vizuri wakati nipo Tanzania, muda mwingine napaona kama nyumbani,”