Home Yanga SC YANGA YATENGA MECHI ZA UBINGWA LIGI KUU BARA

YANGA YATENGA MECHI ZA UBINGWA LIGI KUU BARA


 UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa bado una nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua mzunguko huu wa pili.

 

Yanga ambayo ilianza mzunguko wa kwanza kwa kasi, iligeuka ghafla mzunguko wa pili ambapo chini ya Kocha Cedric Kaze ambaye amefutwa kazi Machi 7, ilicheza mechi 6 na kuambulia ushindi mara moja, sare nne na kupoteza moja.

 

Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Yanga, amesema baada ya timu hiyo kucheza mechi 12 zijazo za ligi ambapo kwa jumla watakuwa wamecheza mechi 35 msimu huu na kubaki tatu kumaliza ligi, tayari itakuwa imesharejea kwenye reli ya kutwaa ubingwa.

 

“Ikiwa utasema kwa sasa tukate tamaa kuhusu ubingwa hilo sio sawa, baada ya mechi 12 za ligi zitatoa picha ya kile ambacho tunakihitaji, mashabiki wasiwe na mashaka, kila kitu kitakuwa sawa na inawezekana.

 

“Mzunguko wa pili ushindani ni mkubwa na kila timu inapambana kusaka ushindi hivyo kinachotakiwa ni kuzidi kupambana na maandalizi mazuri katika mechi zetu, tunachotakiwa ni kupata matokeo chanya, hakuna jambo lingine.”


Yanga ipo nafasi ya kwanza na imekusanya jumla ya pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  WABABE WA SIMBA NA YANGA CAF KUJULIKANA KESHO....DROO KUCHEZESHWA KWA STAILI HII...