Home Simba SC JOASH ONYANGO KUSEPA BONGO, HALI YAKE IPO HIVI

JOASH ONYANGO KUSEPA BONGO, HALI YAKE IPO HIVI

0

 


BEKI kisiki wa Klabu ya Simba, Joash Onyango amesema kuwa yupo vizuri baada ya kupata maumivu Kwenye mchezo wao dhidi ya Al Merrikh. 


Jana Machi 16 wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Al Merrikh,  Onyango alipata maumivu dakika ya 43 na nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni. 


Hali yake ilionekana kuwatisha mashabiki kwa kuwa alitolewa akiwa amebebwa Kwenye machela.


Onyango amesema:”Nipo salama na ninaendelea vizuri natarajia kuelekea Kenya kwa timu ya Taifa,”