Home Simba SC CHAMA AWAPA SIMBA BEKI WA ZAMBIA ILI WAMSAJILI

CHAMA AWAPA SIMBA BEKI WA ZAMBIA ILI WAMSAJILI


NYOTA wa Simba Clatous Chama amewaambia mabosi wake kuwa kaka yake Adrian Chama ana uwezo mkubwa uwanjani kumshinda yeye hivyo wakimpa mkataba atafurahi kucheza naye.

Chama ana miaka 29 kaka yake Chama anayecheza ZESCO United ana miaka 32 na wote wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya Zambia.

Kaka yake Chama, nafasi yake uwanjani ni beki huku mdogo wake Chama anacheza nafasi ya kiungo yupo zake pia timu ya Taifa ya Zambia.

Chama amesema:”Ninajua kwamba kaka yangu ana uwezo mkubwa na anajua mpira hivyo akipata nafasi ya kucheza Simba atafanya vizuri na kuleta changamoto kwa wengine.

“Ninamjua na ninapenda kuwa naye kila mahali hivyo hakuna tatizo ikiwa Simba watamsajili watakuwa wamepata mchezaji mzuri,” .

SOMA NA HII  KIPA MPYA SIMBA HUYU HAPA....JAMAA ANADAKA MPAKA 'MBU'....