Home Simba SC MO DEWJI ‘AUNYOOSHEA KIDOLE’ MKATABA WA SIMBA NA SPORTPESA

MO DEWJI ‘AUNYOOSHEA KIDOLE’ MKATABA WA SIMBA NA SPORTPESA


Mkataba mpya wa udhamani wa Jezi ambao klabu ya Manchested United imesaini na Teamviewer umemfanya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba Mohammed Dewji kuzungumza akionyesha matamanio ya kupata mkataba kama huo kwani ule wa sasa kati yao na Sportpesa hauipi klabu hiyo hata asilimia moja.

“Manchester United imekubali mkataba wa udhamini wa jezi wenye thamani ya $305 milioni kwa miaka mitano. Simba haipati angalau 1% ya kiasi hicho kutoka Sportpesa. Muda utafika wa kuangalia malisho mazuri”

Manchester United has agreed to a $305 million shirt sponsorship contract for 5 years. @SimbaSCTanzania doesn’t get even 1% of that with sports Pesa. Time has come to look out for better pastures.

— Mohammed Dewji MO (@moodewji) March 22, 2021

Simba kwa sasa inadhaminiwa na Sportpesa baada ya kusaini mkataba wa shilingi bilioni 4.96 mwezi Mei mwaka wa 2017 .

Pamoja na kwamba mkataba huo haukuwa wazi sana kwa umma kuhusu udhamini wa jezi, uligusa pia mambo mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo.

Mkataba uliitaka kila mwaka Sports pesa kuipatia Simba zaidi ya shilingi milioni 800 huku mwaka wa mwisho wa mkataba ikipokea bilioni 1 na milioni 80.

Na iwapo itashinda Klabu bingwa Afrika, Sports pesa ingeitengea simba shilingi milioni 250 za ubingwa kama ilivyoipatia shilingi milioni 100 kwa kuchukua ubingwa wa Tanzania msimu uliopita.

SOMA NA HII  NTIBAZONKIZA KASALIMIKA SIMBA...?, UKWELI WOTE HUU HAPA....BENCHIKHA ANAHUSIKA...