“MAMBO mazuri yanakuja Yanga” ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mipango mikubwa ambayo klabu hiyo imeanza kuisuka kwa kushirikiana na Wataakamu wa soka kutokea mataifa ya Afrika Kusini, Latvia, Ghana na Uganda.
Mipango hiyo inakuja muda mfupi baada ya wageni hao kutembelea makao makuu ya klabu hiyo wikiendi iliyopita, na kukutana na viongozi mbalimbali wa Yanga wakiwemo Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa na Mshauri Mkuu wa masuala ya mabadiliko, Senzo Mbatha.
Yanga ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa ambapo wamefanikiwa kukusanya pointi 50 katika michezo yao 23 waliyocheza.
Akizungumzia ujio huo, Senzo amesema: “Tunashukuru kwa ugeni tulioupokea hivi karibuni wa wataalamu wa masuala ya soka kutoka nchi za Latvia, Uganda, Ghana na Afrika Kusini.
“Ugeni huu umetupa wasaa mzuri wa kujifunza na kubadilishana uzoefu, juu ya mambo mengi kuhusiana na mchezo wa soka na ukuaji wa klabu yetu.”