Home Yanga SC MWAMBUSI: TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO

MWAMBUSI: TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini watafanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ambazo ni Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mwambusi amesema kuwa tayari maandalizi yameanza kwa vijana wake na mwendo ambao ameanza nao anaamini watafanya vizuri.

Kocha huyo amechukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mataokeo mabovu kwa timu hiyo kwenye mechi zake za mzunguko wa pili.

“Tayari tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zijazo na tuna amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.

“Uzuri ni kwamba kila mchezaji anakazi ya kutimiza majukumu yake. Kuna mechi za ligi pamoja na kombe la Shirikisho, tutafanya vizuri na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ina pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 ndani ya ligi na watani zao wa jadi Simba wapo nafasi ya pili na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

SOMA NA HII  KAZE: MAKAMBO HAMNA KITU SIKU HIZI...TULITAKA MAYELE APUMZIKE TU...