Home Simba SC ALLY MAYAY: SIMBA NA YANGA ZINATEGEMEANA KATIKA MAFANIKIO

ALLY MAYAY: SIMBA NA YANGA ZINATEGEMEANA KATIKA MAFANIKIO


IMEBAINISHWA kuwa klabu kongwe na kubwa Tanzania Simba na Yanga ambazo zinatajwa kuwa na mashabiki wengi zinategemeana katika maendeleo. 

kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya michezo Tanzania, Ally Mayay Tembele amesema kuwa kila timu imekuwa ikitazama mpinzani wake anafanya nini jambo ambalo linaongeza ushindani kwa timu hizi mbili.

 Ameweka wazi kwa kusema kuwa Klabu ya Azam FC ya Dar ambayo imeweka nguvu kubwa katika uwekezaji ilipoanza kujenga Uwanja wa Azam Complex hakukuwa na shinikizo kubwa la mashabiki wa timu hizo wakihitaji na wao kupiga hatua hiyo ila baada ya Simba kuanza presha imekuwa kubwa.

“Nadhani unaona kwamba wakati ule Azam FC inajenga uwanja wa kisasa ule wa Azam Complex hakukuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa hizi timu mbili kuhitaji kuona timu zao zinafanya hivi.

“Ila baada ya Simba kuanza kujenga uwanja wao na kuuzindua kwa ajili ya kufanyia mazoezi unaona kwamba kumekuwa na presha kubwa na tayari Yanga wameanza mchakato wa kujenga uwanja wao wa mazoezi.

“Hii inamaanisha kwamba hizi timu zote mbili zinategemeana katika kutafuta mafanikio hivyo kwa sasa ni muhimu kila timu ikatafuta mafanikio yake kwa uhalali na kufikia malengo ambayo wamejiwekea,” .

SOMA NA HII  HATIMA YA AISHI MANULA...KUAMULIWA LEO SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI