Home Azam FC PRINCE DUBE: NI MIPANGO YA MUNGU

PRINCE DUBE: NI MIPANGO YA MUNGU


 NYOTA wa kikosi cha Azam FC Prince Dube amesema kuwa yote yanatokea kwa kuwa ni mipango ya Mungu jambo ambalo anashukuru kila wakati.

Ndani ya Azam FC, Dube ni kinara wa utupiaji akiwa ametupia jumla ya mabao 8 katika Ligi Kuu Bara huku kinara wa ujumla akiwa ni John Bocco wa Simba na Meddie Kagere naye pia wa Simba hawa wametupia mabao 9.

Kasi yake ilipungua kwa kuwa alipata majeraha jambo ambalo limemfanya acheze jumla ya mechi 18 za Azam FC kati ya 24 ambazo timu hiyo inayonolewa na George Lwandamina imecheza.

Amekosekana kwenye mechi sita na ametoa jumla ya pasi tano za mabao hivyo jumla amehusika kwenye mabao 13 kati ya mabao 34 ambayo yamefungwa.

Dube amesema:”Yote yanatokea kwa sababu ya mipango ya Mungu, ninawashukuru wote ambao wananiombea na kunikumbuka pia, nitazidi kupambana,”.

SOMA NA HII  AZAM FC YATINGA HATUA YA NUSU FAINALI