Home CAF AS VITA KUTUA TZ KESHO..DJUMA SHABANI HATIHATI KUJA..!!

AS VITA KUTUA TZ KESHO..DJUMA SHABANI HATIHATI KUJA..!!


KIKOSI cha AS Vita kitaingia nchini mchana wa kesho Alhamisi  Aprili Mosi, wakitokea kwao DR Congo na Shirika la ndege ya Ethiopia.

Kikosi hicho kitawasili kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko wa tano Ligi ya mabingwa Afrika katika hatua ya makundi dhidi ya wenyeji wao Simba.

Bahati mbaya katika msafara huo wa AS Vita unaweza kuwakosa wachezaji nyota wawili wa kikosi cha kwanza, Ernest Luzolo na Djouma Shabani.

Luzolo ambaye ni beki wa kushoto na Shabani beki wa kulia wote wa kikosi cha kwanza.

Taarifa kutoka ndani ya AS Vita zineleza wachezaji hao wazaweza kushindwa kuwepo na kikosi cha Simba ambacho kitawasili nchini kutokana wote wamepata majeraha makubwa ya miguu.

“Luzolo na Shabani wote waliumia katika katika timu ya taifa ya Congo na majeraha waliyoyapata ni makubwa ambayo yanaweza kuwaweka nje si chini ya miezi sita,” alisema.

Mmoja wa mawakala wakubwa Congo, Nestor Mutuale alisema kuna taarifa kuwa wachezaji hao hawatakuwepo kutokana na majeraha makubwa ambayo wameyapata katika timu ya taifa.

“Hawawezi kuwepo kwani majeraha ambayo wmeyapata wanaweza kuwa nje ya uwanja hata kwa mwaka mmoja,” alisema Mutuale.

Mutuale ndio wakala ambaye amewaleta nchini, wachezaji watatu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda wote wa Yanga pamoja na Mpiana Monzinzi.

SOMA NA HII  NKANA FC WAGOMA KUFANYIA MAZOEZI UWANJA WA MKAPA