Home Yanga SC BAADA YA KUMALIZANA NA WAGOSI WA KAYA SASA YANGA MIKONONI MWA POLISI

BAADA YA KUMALIZANA NA WAGOSI WA KAYA SASA YANGA MIKONONI MWA POLISI


 BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Machi 4, nguvu kubwa zimeelekezwa kwenye mchezo wa kesho, Machi 7.

Coastal Union ya Tanga maarufu kama Wagosi wa Kaya inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imekuwa ni timu ya kwanza kushinda mbele ya Yanga ambayo ilicheza mechi 21 bila kupoteza.

Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 49 baada ya kucheza mechi 22 kesho itakaribishwa na Polisi Tanzania, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Utachezwa majira ya saa 10:00 ambapo timu zote mbili zina kazi ya kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kurekebisha makosa ambayo yametokea kwenye mechi zao za nyuma.

“Makosa ambayo yametokea kwenye mechi za nyuma tunayafanyia kazi ili kuweza kuwa bora zaidi, kikubwa ni kwamba kila mmoja anahitaji kuona matokeo hata sisi pia tunahitaji kufanya vizuri.

“Mashabiki wazidi kutupa sapoti tunaamini kwamba tutakuwa vizuri na kila kitu kitakuwa sawa hakuna haja ya kukata tamaa,” amesema.

Wapinzani wao Polisi Tanzania kwenye msimamo wapo nafasi ya 8 na pointi zake ni 28.

SOMA NA HII  MRUNDI WA YANGA AWAAHIDI MASHABIKI FURAHA