Home Ligi Kuu COASTAL UNION: YANGA ILIKUWA LAZIMA IFUNGWE KWA NAMNA YOYOTE

COASTAL UNION: YANGA ILIKUWA LAZIMA IFUNGWE KWA NAMNA YOYOTE


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga ambayo imejichimbia kambi yake maeneo ya Mikanjuni, Tanga amesema kuwa ilikuwa lazima Yanga afungwe Mkwakwani kwa kuwa hali ya timu yake ilikuwa ni mbaya.


 Mgunda alikiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na kulipa kisasi cha kupoteza kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo Coastal Union ilifungwa mabao 3-0.

Mgunda alikuwa ni mzawa wa kwanza kuitungua Yanga ambayo ilikuwa imecheza jumla ya mechi 21 bila kupoteza ndani ya uwanja.

Iligonga mwamba rekodi hiyo Machi 4, Uwanja wa Mkwakwani zama za Cedric Kaze ambaye hakuwa na bahati kwenye mzunguko wa pili mpaka kuchimbishwa kazi mazima.

Mgunda amesema kuwa walikubaliana kwamba timu yoyote ambayo ingetia timu Mkwakwani mzunguko wa pili lazima ifungwe.

“Ilikuwa ni lazima Yanga ifungwe hapa Mkwakwani kwa kuwa tulikubaliana kwamba timu yoyote ambayo itashuka nyumbani lazima ifungwe. Hakukuwa na chaguo na wachezaji walielewa somo.

“Nafasi ya 13 ambayo tulikuwa tupo niliwaambia kwamba ni mbaya hivyo hali ilikuwa mbaya kwetu bahati mbaya timu ambayo ilikuwa mbele yetu ni Yanga, hamna namna nawapongeza vijana wamepambana na pointi tatu tumechukua.

“Ushindi huo ni kazi kwetu kuongeza nguvu ya kupambana kwenye mechi zetu zijazo, mashabiki wazidi kutupa sapoti kazi bado ipo,” .

 

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....POLISI TZ WATAMBA 'KUIPELEKEA MOTO WA KUTOSHA' SIMBA...